UIMARISHAJI MIUNDOMBINU YA MAJITAKA KIPAUMBELE SINZA - MWENGE

Kazi ya uboreshaji Usafi wa Mazingira katika eneo la Sinza A hadi Mwenge ikiendelea chini ya watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ili kuhakikisha wananchi wanakua katika mazingira safi na salama.
Uboreshaji huo wa Usafi wa Mazingira umehusisha ujenzi wa mifuniko ya chemba ili kutoruhusu taka ngumu kuingia katika mifumo ya majitaka na kuisababisha kuziba na kuchafua mazingira.
Sambamba na hilo uboreshaji wa Usafi wa mazingira umeenda sambamba na kurekebisha na kubadili bomba chakavu la majitaka inchi 6 mtaa wa Kudewa, Mwenge ili kudhibiti uvijaji wa mara kwa mara.
Mamlaka inawakumbusha wananchi wote kutunza miundombinu ya majitaka na kuwa wakwanza kutoa taarifa pale wanapoona uhujumu wa miundombinu hii kama vile kutupa taka ngumu pamoja na wizi wa mifuniko ya chemba.