UIMARISHAJI WA HUDUMA YA MAJI KIWALANI, BUZA NA AIRPORT

Kazi ya kukagua pamoja na kutoa upepo katika miundombinu ya usambazaji maji imetekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika maeneo ya kwa Gude na Lumo kata ya Kiwalani kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Kiwalani, Lumo, Kigilagila, Buza na Airport
Mamlaka kupitia Mkoa wa kihuduma DAWASA - Temeke inaendelea na zoezi la ufuatiliaji wa hali ya maji katika maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Mtoni, Ruvu Chini, Ruvu Juu pamoja na Visima vya Kigamboni kwa lengo la kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa msukumo mzuri.
Utoaji wa upepo ni zoezi muhimu kufanyika kwa lengo la kuondoa hewa ambayo huingia katika bomba, wakati hakuna maji na kusababisha huduma ya maji kupatikana kwa msukumo mdogo.