USOMAJI MITA SHIRIKISHI UKONGA
15 Jun, 2024

Watumishi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (DAWASA) wa Mkoa wa Kihuduma Ukonga wakiendelea na zoezi la usomaji mita shirikishi katika maeneo ya mbalimbali ya mkoa wa Kihuduma.
Zoezi la usomaji mita linaendelea kutekelezwa na DAWASA kwa kuwafikia wateja na kushirikiana katika usomaji wa mita za maji kwa lengo la kuboresha huduma. Aidha, zoezi hili huenda sambamba na utoaji wa elimu mbalimbali juu ya huduma zinatolewa na DAWASA ikiwemo uhakiki wa usomaji mita, njia za malipo na mawasiliano rasmi ya Mamlaka.