USOMAJI MITA SHIRIKISHI WAENDELEA UBUNGO
Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mkoa wa Kihuduma Ubungo wameendelea na zoezi la usomaji mita kwa kushirikiana na wateja katika maeneo ya Mbezi, Saranga, Makabe, King'ongo, Kimara Baruti pamoja na Malamba Mawili.
Zoezi la usomaji mita linaendelea kutekelezwa na Mamlaka katika kata tano za wilaya ya Ubungo zenye wateja takribani 37,834 kwa lengo la kuwafikia na kushirikiana nao katika usomaji wa mita za maji pamoja na kuboresha huduma.
Akizungumzia hatua hiiyo, Afisa Biashara wa DAWASA Ubungo, Boniphace Ndama amesema zoezi hilo linaendelea kikamilifu japo kutokana na changamoto za hali ya hewa kumekuwa na changamoto za usomaji wa pamoja.
"Tunaendelea na usomaji mita kwa kushirikiana na wateja katika maeneo mbalimbali japo muitikio umekuwa mdogo kiasi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha tunawashukuru wateja wanatupa ushirikiano bila kujali changamoto ya hali ya hewa," amesema.
Aidha, kupitia zoezi hili linakwenda sambamba na utoaji wa elimu mbalimbali juu ya huduma zinazotolewa na DAWASA ikiwemo uhakiki wa usomaji mita, matumizi sahihi ya maji, njia za malipo na mawasiliano ya Mamlaka pamoja na kutatuliwa changamoto za hapo kwa hapo ikiwa ni uboreshaji zaidi wa huduma.
