USOMAJI NA UHAKIKI WA MITA UNAENDELEA TABATA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma Tabata unaendelea kuwakumbusha wateja juu ya umuhimu wa usomaji mita shirikikishi na uhakiki wa usomaji pindi wanapopata ujumbe mfupi baada ya zoezi la usomaji.
Afisa Biashara wa DAWASA Tabata, Ndugu Neema Mosha amesema zoezi la usomaji wa mita kwa kushirikiana na wateja linaendelea sambamba na uhakiki wa usomaji ambapo wateja wanapata nafasi ya kuhakiki kabla ya kuandaliwa bili yake hii husaidia kupunguza malalamiko pindi bili zinapotumwa kwa wateja.
"Zoezi la usomaji mita bado linaendelea na baadhi ya wateja tayari wameshapokea jumbe fupi za uhakiki wa usomaji, tunatoa rai kwa wateja wetu ni muhimu kuhakiki usomaji wako na kutoa taarifa kama kuna changamoto kupitia mawasiliano yetu rasmi au kufika katika ofisi zetu ili kutatua changamoto hizo kabla ya bili kutayarishwa" amesema Ndugu Mosha
Ndugu Mosha amesisitiza ushirikiano kati ya wateja na Mamlaka ni muhimu hivyo anaendelea kuwasihi wateja kutoa ushirikiano kwa watumishi pindi wanapopita katika makazi yao.
Mkoa wa kihuduma DAWASA Tabata una jumla ya wateja takribani 296,572 na unahudumia Kata za Tabat, Liwiti, Segerea, Kimanga, Kisukuru, Makuburi, Vingunguti, Kipawa, Mnyamani na Bonyokwa.