VIFAA VYA MAUNGANISHO MAPYA VYAWASILI GOBA, MATOSA NA TEGETA “A”
05 Jul, 2024

Vifaa vya maunganisho mapya kwa kwa wakazi wa maeneo ya Goba, Tegeta A, Matosa, Makabe, Mlalakuwa vimewasili kwa ajili ya kuwahudumia Wananchi waliiomba na kukamilisha taratibu za upatikanaji huduma ya Majisafi.
Zoezi la kugawa vifaa hivyo linaendelea katika ofisi za DAWASA MAKONGO na zaidi ya Wateja 300 wanategemea kuunganishwa na huduma ya Majisafi.
Zoezi hilo linaenda sambamba na utoaji wa elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, njia rasmi za kuwasiliana na Mamlaka na malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.
Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0736602601 (DAWASA Makongo)