Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
WAKAZI 100 WA KILUVYA - MSAKUZI KASKAZINI KUANZA KUFURAHIA HUDUMA YA MAJISAFI
20 Nov, 2024
WAKAZI 100 WA KILUVYA - MSAKUZI KASKAZINI KUANZA KUFURAHIA HUDUMA YA MAJISAFI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma DAWASA Kibamba imeendesha zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya Majisafi kwa wateja wa maeneo ya Kiluvya, Gogoni, Hondogo, Kwembe, Kingazi  A, Kingazi  B, Malamba mawili, Mpiji Magohe, Luguruni, Kibwegere, Mbezi kwa Yusuph, Mshikamano Msakuzi Kaskazini, na Makurunge, ili wanufaike na jitihada za Serikali za kuhakikisha wanapata Majisafi.

Mbali na zoezi la utoaji wa vifaa hivyo, DAWASA Kibamba imetoa elimu mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na Mamlaka.

Jumla ya wateja wapya 100 wa maeneo hayo wanaenda kunufaika na huduma ya majisafi baada ya kukamilika kwa zoezi la maunganisho.

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) au 0734 460 022 DAWASA Kibamba.