Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
WAKAZI HAILE SELASSIE WABORESHEWA MIUNDOMBINU
30 Sep, 2025
WAKAZI HAILE SELASSIE WABORESHEWA MIUNDOMBINU

Kazi ya matengenezo ya bomba la inchi 6" ikitekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA - Kinondoni) katika mtaa wa Haile Selassie kata ya Msasani Wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kudhibiti upotevu wa maji uliosababishwa na kupasuka kwa bomba hilo.

Maboresho hayo yataboresha upatikanaji wa maji kwa wakazi takribani 450 wa maeneo ya Haile Selassie, Chole, Lincoln, Ruvu, Kaole, Mawenzi na Katoke.