WAKAZI KIGOGO WAITWA MAUNGANISHO YA MAJISAFI

Wakazi wa Mtaa wa Kigogi, kata ya Kisarawe II katika Wilaya ya Kigamboni wamehimizwa kujitokeza kuunganishiwa huduma ya Majisafi baada ya kukamilika kwa Mradi wa Maji Kigogo uliotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) unaolenga kuhudumia Wakazi takribani 6,800
Akizungumza katika zoezi la kuandikisha wateja wapya waliojitokeza kuomba huduma ya Majisafi, Afisa huduma kwa Wateja,
DAWASA Kigamboni, Ndugu Flora Joseph amesema mradi wa Majisafi Kigogo umetekelezwa kwa lengo la kusogeza huduma karibu na kuwaasa wananchi kujitokeza kwa wingi kuomba huduma.
"Tumefungua dawati la huduma kwa wateja katika Mtaa wa Kigogo Kigamboni kwa lengo la kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kujiunga na huduma ya Majisafi kupitia mradi huu wa Kigogo, mradi umekamilika na watendaji wa DAWASA watakuwa hapa kwa muda hivyo niwasihi wananchi kujitokeza kupata elimu na kujiunga na huduma ili kuweza kutumia majisafi na salama" ameeleza Frola.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kigogo ndugu, Ramadhani Mtawa ameipongeza DAWASA kwa utaratibu wa kusogeza huduma karibu kupitia Madawati ya huduma kwa wateja kwani hurahisisha zaidi upatikanaji wa taarifa za huduma za Majisafi.
Utekelezaji wa Mradi wa Majisafi Mtaa wa Kigogo umehusisha ulazaji wa mabomba ya ukubwa tofauti kuanzia inch "1.5, “2, “4, “6, “8 kwa umbali wa kilomita 20