Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
WAKAZI MBAGALA ZAKHIEM WABORESHEWA HUDUMA YA MAJISAFI.
10 Mar, 2025
WAKAZI MBAGALA ZAKHIEM WABORESHEWA HUDUMA YA MAJISAFI.

Kazi ya uboreshaji wa upatikanaji wa huduma ya majisafi katika Mtaa wa Kokomo, Zakhiem ikiendelea kutekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa kihuduma Mbagala.

Maboresho hayo yamehusisha ulazaji wa bomba za inchi 6 kwa umbali wa mita 350 na yamelenga kuimarisha hali ya upatikanaji huduma ya majisafi kwa wakazi wa Mtaa wa Zakhiem, Kata ya Mbagala Kuu ambao walikuwa wanapata huduma ya maji kwa msukumo mdogo na baada ya maboresho haya hali ya msukumo wa maji itaongezeka.