WAKAZI WA MAILIMOJA HADI VISIGA KUPATA HUDUMA YA MAJISAFI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma DAWASA Kibaha inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya majisafi kwa wateja wa maeneo ya Mailimoja, Sofu, Mwanalugali, Mkuza, Msangani, Kidenge, Mbwate, Awendapole, Simbani, Galagaza, Miembe saba, Kongowe, Misigugusugu, na Visiga ili wanufaike na jitihada za Serikali za kuhakikisha wanapata maji.
Sambamba na zoezi la utoaji wa vifaa hivyo, DAWASA Kibaha imetoa elimu mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za kimawasiliano, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na Mamlaka.
Zaidi ya wateja wapya 100 wa maeneo hayo wataanza kunufaika na huduma ya majisafi baada ya kukamilika kwa zoezi la maunganisho.
Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 ( Bure ) au 0735 451 875 DAWASA Kibaha.