WAKAZI ZAIDI YA 400 SINZA E NA D WAIMARISHIWA HUDUMA YA MAJI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na kazi ya uboreshaji wa miundombinu ya mabomba ya Maji ili kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wateja zaidi ya 400 waliopo Mtaa wa Mwibula, kata ya Sinza E Wilaya ya Ubungo.
Maboresho hayo yanahusisha kazi ya kuunganisha njia ya ziada ya bomba la maji kutoka kwenye toleo la bomba kubwa la inchi 33" na kuingiza katika bomba la inchi 3" kwa umbali wa mita 500.
Kazi hii ya maboresho ya miundombinu ya maji inatekelezwa na DAWASA Mkoa wa kihuduma Magomeni.
Kukamilika kwa maboresho hayo kutaongeza upatikanaji wa maji na kuimarisha huduma kwa wateja 400 kwa wakazi wa maeneo ya mtaa wa Mwibula, mtaa wa White Inn, Iteba Secondary, mtaa wa Vick Kamata, Vunja bei, Kanisa la wasabato na Shule ya Msingi Sinza D.
