Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
WAKAZI ZAIDI YA 900 MIKOCHENI WAIMARISHIWA HUDUMA YA MAJI
28 Jan, 2026
WAKAZI ZAIDI YA 900 MIKOCHENI WAIMARISHIWA HUDUMA YA MAJI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na kazi ya uboreshaji wa miundombinu ya mabomba ya Maji ili kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wateja zaidi ya 900 waliopo Mtaa wa Mwalimu Nyerere, kata ya Mikocheni Wilaya ya Kinondoni.

Maboresho hayo yanahusisha kazi ya kuunganisha njia ya ziada ya bomba la maji kutoka kwenye kipenyo cha inchi 6 na kuingiza katika bomba la inchi 10 kwa umbali wa kilomita 3.

Kazi hii ya maboresho ya miundombinu ya maji inatekelezwa na DAWASA Mkoa wa kihuduma Kinondoni.

Kukamilika kwa maboresho hayo kutaongeza upatikanaji wa maji na kuimarisha huduma kwa wateja 970 kwa wakazi wa maeneo ya mtaa wa Asmara, mtaa wa Misholi, mtaa wa Msonge, mtaa wa kitambaa, TMJ Hospital, Mayfair Hotel pamoja na Shopper Plaza.