WANANCHI KIBAMBA KUNUFAIKA NA MABORESHO HUDUMA YA MAJI
14 Aug, 2025

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam DAWASA, mkoa wa kihuduma Kibamba wakiendelea na kazi mbalimbali za uboreshaji huduma ya maji katika maeneo ya Kwembe, Msigani, Kiluvya Magari saba pamoja na Malamba mawili.
Maboresho hayo yanajumuisha kupambana dhidi ya upotevu wa maji kwa kudhibiti mivujo pamoja Kuongeza msukumo wa maji katika maeneo yenye msukumo mdogo wa maji.
Ni kipaumbele cha Mamlaka kutoa huduma ya majisafi yenye ubora wa viwango vya juu kwa wananchi inayowahudumia ili kuchochea ustawi na maendeleo ya jamii.