WATEJA 53 WA KIHARAKA - KEREGE WAUNGANISHIWA MAJISAFI
20 Nov, 2024

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa Kihuduma DAWASA Mapinga imeendesha zoezi la ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya kwa wateja 53 wa maeneo ya Vikawe, Kimele, Kibosha, Kiharaka, Kiembeni, Kerege, Mtambani na udindivu.
Zoezi hili la utoaji wa Vifaa vya maunganisho mapya kwa wateja linaendelea katika Mikoa yote ya kihuduma Dar es Salaam na Pwani kwa wananchi walioleta maombi yao kuanzia mwezi wa septemba na Oktoba 2024.