WATUMISHI DAWASA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO MAADHIMISHO YA 9 DESEMBA
03 Dec, 2024

Mwakilishi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA), Mhandisi Lydia Ndibalema akikabidhi bendera ya uwakilishi kwa Watumishi watakaopanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya Sherehe za Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania.
DAWASA ni miongoni mwa Taasisi zitakazoshiriki kampeni hii iliyopewa jina la Twende zetu kileleni inayoratibiwa na Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA)