WATUMISHI WANAWAKE DAWASA WAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE DUNIANI

Watumishi mbalimbali wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) wameungana na wenzao kote Duniani kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake duniani ambapo katika Mkoa wa Dar es salaam maadhimishi yamefanyika katika viwanja vya wazi leaders club.
Aidha baadhi wa watumishi wanawake wa DAWASA wameadhimisha sikukuu hiyo katika Mkoa wa Pwani maadhimisho yaliyofanyika katika Wilaya ya Mkuranga.
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake duniani Kitaifa yamefanyika katika Mkoa wa Arusha na kuhudhuriwa na wanawake mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali Nchini huku Mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake duniani kwa mwaka 2025, yamebeba kauli mbiu isemayo "Wanawake na Wasichana 2025, Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji"