Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
WAZIRI AWESO AFURAHISHWA NA HUDUMA KWA WATEJA DAWASA
02 Jul, 2024
WAZIRI AWESO AFURAHISHWA NA HUDUMA KWA WATEJA DAWASA

Waziri Aweso amefurahishwa na kauli njema kutoka mmoja wa wahudumu kwa wateja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) wakati wa ziara yake inayoendelea Jijini Dar es salaam alipopiga namba hiyo 0800110064 inayopatikana bila malipo na kuongea na mhudumu kwa weledi zaidi kwa kuhakikishiwa huduma bila usumbufu.

Amefanya zoezi hilo akiwa katika  Mtaa wa Kibululu Kata ya Goba Wilayani Ubungo alipokutana na Wananchi wakati wa kusikiliza changamoto za huduma ya Maji.