WAZIRI AWESO ASISITIZA WANANCHI KUPATA MAJI KWA MRADI WA BANGULO
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhakikisha uwekezaji wa mradi mkubwa wa maji wa Dar es Salaam ya Kusini (Bamgulo) unaleta manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi walengwa wa mradi huu.
Akizungumza katika siku ya pili ya ziara yake alipofika kukagua maendeleo ya mradi huu, Mhe. Waziri amesema kuwa kwa kuwa mradi umeshakamilika, kazi iliyopo ni kuhakikisha wananchi wote wanapata maji kwa kufanya kazi ya maunganisho kwa kasi.
Ameongeza kuwa mradi huu umetekelezwa mahususi kwa lengo la kuhakikisha maeneo yote ya Jimbo la Segerea, Ilala, Ubungo, Kibamba na Temeke wanapata maji kwa uhakika.
Ameitaka Mamlaka kuweka kambi katika eneo la wananchi kwa lengo la kuwaunganisha wateja na huduma ya majisafi.
