TAARIFA KWA UMMA - KUKAMILIKA KWA MABORESHO MTAMBO WA RUVU JUU NA KUREJEA KWA HUDUMA YA MAJI
TAARIFA KWA UMMA
KUKAMILIKA KWA MABORESHO MTAMBO WA RUVU JUU NA KUREJEA KWA HUDUMA YA MAJI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu juu kuwa, maboresho katika mfumo wa umeme katika Pampu za kusukuma maji yamekamilika na huduma ya maji imeanza kurejea katika baadhi ya maeneo kwa Wakazi wa Kibaha hadi Kisarawe.
DAWASA inawahakikishia Wananchi kuwa huduma inaendelea kuimarika katika maeneo mengine na hadi kesho, Oktoba 23,2024 huduma itasambaa katika eneo lote linalohudumiwa na Mtambo wa maji Ruvu juu.
Maeneo ambayo huduma inaendelea kuimarika ni pamoja na;
Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, na Kiluvya, Kibamba Shule, Kibamba kwa mangi, Kibamba CCM, Kwembe na baadhi ya maeneo ya Malamba, Bonyokwa, Kwa Msuguli, Kimara Temboni, Luguluni, Kibanda cha mkaa, Kimara matangini
Maeneo ambayo huduma itarejea katika hali yake ya kawaida kufikia kesho,Oktoba 23,2024 ni;
Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi Kimara, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Changanyikeni, Makongo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe.
Kwa changamoto yoyote wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au 0735 202-121 (WhatsApp Tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano