TAARIFA KWA UMMA - MATENGENEZO YA DHARURA YA BOMBA KUBWA CHANGANYIKENI NA MAKONGO
TAARIFA KWA UMMA
MATENGENEZO YA DHARURA YA BOMBA KUBWA CHANGANYIKENI NA MAKONGO
22.9.2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu Wateja na Wananchi wa maeneo ya Changanyikeni na Makongo kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya Maji kwa muda wa Saa 10.
Muda: Septemba 22, 2026 kuanzia Saa 7 Mchana hadi Saa 4 Usiku.
Sababu: Matengenezo ya dharura ya bomba la inchi 16 katika eneo la Changanyikeni.
Maeneo yatakayoathirika ni;
Mtipesa, Kibululu, Ronda Mnalani, Kona Ajabu, Kingstone, Kwa Mongela, Shule ya Sekondari Makongo, Njia Panda Ronda, Kwa Njau, Barabara ya Mtaa wa Ng'ombe, Mtaaa wa Atido, Downvialley, Kwa Diwani, Kwa Uombe na Serikali ya Mtaa Makongo Orlex, Mambosasa, Mbezi Madukani, St. Columbus, Chongoro, Kanisa Katoriki, Kwa Mlaki, Saiberia na George Washington.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Endelea kuwasiliana nasi kupitia Kituo cha huduma kwa wateja DAWASA 181 (bila malipo) au 0735 202 121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
