TAARIFA KWA UMMA - UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WATEJA BAGAMOYO HADI KATIKATI YA JIJI
TAARIFA KWA UMMA
UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WATEJA BAGAMOYO HADI KATIKATI YA JIJI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa uzalishaji maji Ruvu Chini kuwa, kutakuwa na ukosefu wa Huduma ya maji kwa wastani wa Saa 12 kila siku kwa siku za Jumamosi 23.11.2024 na Jumapili 24.11.2024
Muda: Saa 3 Asubuhi hadi saa 12 Jioni
Sababu: Kuruhusu Matengenezo ya miundombinu itakayosaidia kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme katika Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Maeneo yatakayoathirika ni;
Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Kunduchi, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo - Kikuu Dar, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya mji.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au 0735 202-121(WhatsApp tu )
Imetolewa na
Everlasting Lyaro
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano