TANGAZO LA DHARURA - UPUNGUFU WA UZALISHAJI MAJI MTAMBO WA RUVU JUU
TANGAZO LA DHARURA
UPUNGUFU WA UZALISHAJI MAJI MTAMBO WA RUVU JUU
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu juu kuwa, kumekuwa na upungufu wa huduma ya maji kutokana na matengenezo ya mfumo wa umeme unaoendesha Pampu za kusukuma Maji Mtamboni.
Muda Oktoba20, 2024 kuanzia Saa 5 Asubuhi hadi Saa 2 Usiku.
Maeneo yatakayoathirika na upungufu huu ni;
Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Segere, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au 0735 202-121 (WhatsApp Tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano