TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI PANGANI, HALMASHAURI YA MJI KIBAHA MKOANI PWANI
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI PANGANI, HALMASHAURI YA MJI KIBAHA-MKOA WA PWANI
TAREHE 24.11.2023
1.0 Utangulizi
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inatarajia kutekeleza mradi wa maji katika maeneo ya Pangani na (kibaha-msufini, lulanzi, TAMCO) katika Halmashauri ya Mji Kibaha-Mkoa wa Pwani, ikiwa ni muendelezo wa jitihada zake za kuboresha huduma ya maji katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya upatikanaji wa maji.
Utekelezaji wa mradi huu utahusisha ujenzi wa kituo cha kusukuma maji kichokuwa na tanki la kupokelea maji lenye ujazo wa 540m³ na zitafungwa pampu tatu kwa ajili ya kusukuma maji kupeleka kwenye tanki kuu la kuhifadhia maji lenye ujazo wa 6000m³ litakalojengwa sambamba na ulazaji wa bomba wenye jumla ya kilometa 18.7 ikiwa inahusisha bomba la kupeleka maji kwenye tenki (Raising main) ambapo utahusisha Ulazaji bomba la chuma lenye kipenyo cha inchi 12 (DN300) pamoja na ujenzi wa mabomba ya kusambaza maji yenye vipenyo ya DN200-DN90 .Chanzo cha maji ni kutoka kwenye bomba la chuma la inchi 24 (DN600) linalotoa maji mtambo wa Ruvu Juu eneo la Msufini kuelekea kwenye tenki maeneo ya Bandari na kibaha-msufini na lulanzi.
Mradi huu utakuwa na uwezo wa kusafirisha maji kiasi cha lita za ujazo milioni tano nukta mbili kwa siku ambazo zitatosheleza mahitaji ya Bandari na Wananchi 14,868 (ambayo ni mahitaji ya kipindi cha miaka 20 ijayo) wa maeneo ya Pangani na (kibaha-msufini, lulanzi, TAMCO).
Mradi huu ni miongoni mwa miradi ya kimkakati iliyopangwa kutekelezwa na DAWASA kwa mwaka 2023/2024 ili kuweza kukidhi agizo la Serikali la kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 upatikanaji wa huduma ya maji unafikia 85% na 95% kwa maeneo ya vijijini na mijini sawia.
2.0 Gharama ya mradi
Mradi huu utagharimu jumla ya Tsh. 9,806,116,567.57 utatekelezwa kwa kutumia fedha inayotokana na makusanyo ya ndani ya DAWASA na kusimamiwa na wahandisi wa ndani. Gharama ni pamoja na VAT.
3.0 Utekelezaji wa mradi
Mradi huu usanifu ulisha kamilika na utatekelezwa rasmi utaanza kwenye mwaka ujao wa fedha 2023/2024. Zoezi la ufuatiliaji wa kina (detailed survey) maeneo litakamopita bomba unaendelea pamoja na maeneo yatakapojengwa kituo cha kusukumia maji na Matangi ya kuhifadhia maji kwaajili ya kuyatwaa.
4.0 Hatua ya utekelezaji ilipofikia
Utekelezaji wa mradi kwa ujumla umefikia asilimia 100 kwenye usanifu.
5.0 Faida za mradi
Kuondoa kero ya upatikanaji maji kwa wakazi 14,868 katika maeneo ya kibaha-msufini, lulanzi, TAMCO na Pangani.
