Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
Vifaa vya Usafi wa Mazingira
Vifaa vya Usafi wa Mazingira

FAHAMU VITUO VYA HUDUMA KWA UMMA

(Public Sanitary Service Point)

UTANGULIZI

Mradi wa ujenzi wa vyoo vya umma ni mradi uliotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) chini ya ufadhili wa mdau wa maendeleo Benki ya Dunia kwa lengo la kuboresha hali ya usafi wa mazingira katika maeneo yenye msongamano wa watu hususani katika masoko, maeneo ya umma na vituo vya daladala.

Mradi huu unatekelezwa na DAWASA kwa ushirikiano na halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam. Mradi huu umetekelezwa katika maeneo 30 katika Mkoa wa Dar es Salaam kama ifuatavyo:

Wilaya ya Kigamboni vyoo 5 vilivyopo maeneo ya, Kibada, Geza Kituo Cha Mabus, Buyuni,Tundwi songani na Geza soko la mazao.

Wilaya ya Temeke vyoo 6 vilivyopo maeneo ya

Toangoma, Tandika Sokoni, Mbagala Kampochea na Mbagala Stand, Sulele Mbande.

Wilaya ya Ilala vyoo 6 vilivyopo maeneo ya Chanika Videte, Kimanga Kituo cha Mabasi, Kipunguni Sokoni, Kigogo fresh, Posta ya zamani na Chanika Zingiziwa.

 

Wilaya ya Kinondoni vyoo 7 vilivyopo maeneo ya Coco Beach, Mwananyamala, Mwanamboka, Bunju Sokoni, Bunju Stand, Magomeni Gardeni, Mbweni Mpiji Sokoni.

Wilaya ya Ubungo vyoo 6 katika maeneo ya Shekilango Sokoni, Mawasiliano Sokoni, Mabibo External, Mloganzila Kituo cha Magari, Manzese Sokoni, na Mbezi luis.

UTEKELEZAJI WA MRADI

Mradi huu umetekelezwa na mkandarasi kampuni ya Helpdesk Engineering Tanzania Limited.

Maendeleo ya mradi: Hadi kufikia Januari 2024, mradi umefikia asilimia 99% ya utekelezaji wake.

Kazi ya ukaguzi wa mwisho na makabidhiano inaendelea kati ya DAWASA, Mkandarasi na Mhandisi mshauri na uendeshaji utaanza kufanyika katika vyoo vilivyokabidhiwa.

MAJARIBIO YA AWALI YA MRADI HUU

Jumla ya vyoo 5 vimeanza kutumika kama majaribio (Pilot) ili kubaini fursa na changamoto katika uendeshaji.

Vyoo hivyo vya majaribio ni vilivyopo Cocoa beach, Shekilango Sokoni, Mbagala Kapochea, Mbagala Stand na Manzese

Sokoni.