💙 HERI YA SIKU YA WANAUME DUNIANI! 🌍
20 Nov, 2026
Pakua
💙 HERI YA SIKU YA WANAUME DUNIANI! 🌍
Katika kuadhimisha Siku ya Wanaume Duniani, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa wanaume katika kujenga familia imara, jamii yenye ustawi na taifa lenye maendeleo endelevu.
💧 Tunawahamasisha wanaume wote kuwa mfano bora katika matumizi sahihi na ya uangalifu wa maji, kuzuia upotevu wa maji na kuwafundisha watoto wetu umuhimu wa kutunza rasilimali hii muhimu.
👨👧 Malezi bora huanza kwa vitendo. Baba anapomfundisha mtoto kutumia maji kwa uangalifu, anajenga kizazi kinachothamini na kulinda rasilimali ya maji kwa maisha ya sasa na vizazi vijavyo.
DAWASA – Maji Safi kwa Maisha Bora! 💙
