Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA KUIMARISHA USTAWI WA WATUMISHI KUPITIA ELIMU YA AFYA
20 Nov, 2026
DAWASA KUIMARISHA USTAWI WA WATUMISHI KUPITIA ELIMU YA AFYA

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wanatarajiwa kunufaika na elimu ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza pamoja na Virusi vya UKIMWI (VVU), kupitia mafunzo ya Waelimisha Rika yanayolenga kuongeza uelewa na kuimarisha ustawi wao.

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa DAWASA, Bernadetha Mwabusila, katika Makao Makuu ya mamlaka hiyo yaliyopo Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.

Yametolewa na mkufunzi Juliana Ntukery kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa lengo la kuwajengea uwezo Waelimisha Rika kuhusu mbinu na miongozo sahihi ya kutoa elimu ya afya kwa watumishi wenzao.

Kupitia mafunzo hayo, washiriki wanatarajiwa kupata ujuzi utakaowawezesha kutoa elimu kuhusu namna ya kujikinga na kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza pamoja na VVU.

Jitihada hizo ni sehemu ya mpango wa DAWASA wa kuimarisha ustawi wa watumishi kwa kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya afya, hatua inayolenga kuchochea tabia za kujikinga na magonjwa na kujenga mazingira bora ya kazi yenye watumishi wenye afya.