IFIKAPO MWAKA 2050 HUDUMA YA MAJISAFI NA SALAMA KUWAFIKIA WATANZANIA WOTE

IFIKAPO MWAKA 2050 HUDUMA YA MAJISAFI NA SALAMA KUWAFIKIA WATANZANIA WOTE
Ifikapo Mwaka 2050 huduma ya Majisafi na salama kuwafikia Watanzania wote.
Dira ya awali (2000-2025) ililenga kuwa watu waishio vijijini wanapata Majisafi kutoka asilimia 50 Mwaka 2000 hadi kufikia asilimia 85 Mwaka 2025 na watu waishio mjini wanapata maji kutoka asilimia 50 Mwaka 2000 kufikia asilimia 95 ifikapo Mwaka 2025.
Mpaka Desemba 2022 , 77% ya watu waishio vijijini walipata huduma ya Majisafi na salama na 88% wakazi wa mjini walikuwa wamefikiwa na huduma ya maji.
Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan upatikanaji wa maji mijini umeongezeka kutoka asilimia 84 hadi asilimia 91.6 na vijijini kutoka asilimia 70.1 hadi asilimia 85
Wakati Rais Samia anaingia madarakani, huduma ya Maji ilikuwa imefika kwa Vijiji 5,258, hadi kufika mwaka 2025 vijiji 10,779 vilikuwa vimefikishiwa huduma ya Maji sawa na ongezeko la vijiji 5,521.
Kutokana na mwenendo huo upatikanaji wa maji unatarajiwa kufikia asilimia 100 ifikapo mwaka 2050.