Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
PONGEZI - MHANDISI MKAMA BWIRE, KAIMU AFISA MTENDAJI MKUU DAWASA
04 Jul, 2024 Pakua

Mhandisi Mkama Bwire ameteuliwa kushika nafasi ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) katika kikao maalum cha Waziri wa Maji na Bodi ya Wakurugenzi DAWASA kilichofanyika leo tarehe 03 Julai, 2024 ofisi za DAWASA Dar Es Salaam.

Mhandisi Bwire ni Mtumishi wa Wizara ya Maji ambae amehudumu kama Mhandisi wa Maji katika Halmashauri ya Kibaha, 
Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) 
na hadi anapokea jukumu hili alikua ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini katika  Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)