DHAMIRA YA RAIS SAMIA YATIMIA , PAMPU ZA MAJI DAR ES SALAAM ZIMEKAMILIKA
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso ametembelea kiwanda cha utengenezaji Pampu za Maji KSB Shangai Pump na kushuhudia ukamilishaji wa Pampu za Mitambo ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) itakayosaidia kupunguza changamoto ya Maji
Pampu hizo kubwa ni kwa ajili ya maboresho ya mitambo ya Ruvu juu na Ruvu chini kwa kuweka pampu mpya na kuondoa za zamani husababisha msukumo mdogo na hata kukosekan maji ya uhakika Dar Es Salaam na Pwani.
Gharama ya pampu hizo ni shilingi bilioni 16.5, ikijumuisha na ufungaji, ambazo zote zimetolewa na Serikali ya Tanzania na kazi ya ufungaji inatarajia kukamilika ifikapo Juni 2026.
Mara baada ya mabadiliko ya pampu hali ya huduma ya Maji inatarajiwa kuboreshwa na kuwa ya uhakika zaidi.
Katika ziara hiyo, Waziri Aweso ameshuhudia majaribio ya mwisho ya awamu ya pili ya Pampu hizo ambapo amejiridhisha na aina, viwango na uwezo wake na kuruhusu mzigo usafirishwe kuleta nchini Tanzania mara moja baada ya matengenezo yake kukamilika.
Aidha, awamu ya kwanza yenye jumla ya Pampu nne ilishakamilika na tayari zimeshawasili nchini na kazi ya ufungaji imeanza.
Ununuzi wa pampu hizi ni hatua za makusudi na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Sululu Hassan kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa Dar Es Salaam na Pwani kupitia Wizara ya maji.
