TAHADHARI YA EL - NINO
TAHADHARI YA EL - NINO
Dondoo muhimu ya ulinzi Miundombinu ya Maji
1. Kuwa na vyombo vikubwa vya kutosha vya kuhifadhi Maji endapo kutatokea changamoto katika uzalishaji uwe na akiba ya kutumia.
2. Hakikisha miundombinu ya Mabomba inayopeleka Maji katika eneo lako imefukiwa vyema ardhini ili kulinda dhidi ya kusombwa au kufukuliwa kutokana na Maji mengi ya Mvua.
3. Epuka shughuli za Kilimo au uchimbaji katika maeneo ambayo miundombinu ya Maji imepita.
4. Usielekeze Maji ya mvua katika Miundombinu ya Majitaka kwani itaelemewa na kufurika hivyo kusababisha uchafuzi wa Mazingira.
5. Epuka utupaji taka ngumu katika miundombinu ya Majitaka ikiwemo katika chemba ili kuruhusu mifumo ifanye kazi kwa ufanisi.
6. Kumbuka kuhifadhi na kutumia namba 181 (huduma kwa Mteja DAWASA) kwa msaada wa haraka wa huduma za Maji.
