Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA MIONGONI MWA WASHIRIKI TUKIO LA ‘MWANAMKE NJOO TUONGEE’
27 Sep, 2026
DAWASA MIONGONI MWA WASHIRIKI TUKIO LA ‘MWANAMKE NJOO TUONGEE’

Sehemu ya Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakishiriki katika tukio la Mwanamke Njoo Tuongee lililoandaliwa na Taasisi ya Hope for All initiative kwa lengo la kujadili na kuhamasisha masuala mbalimbali yanayomhusu ustawi wa Mwanamke katika nyanja mbalimbali ikiwemo Afya ya akili, ukuaji wa Taaluma (Career develeopment) na uwiano kati ya kazi na maisha.

Ushiriki wa DAWASA unaakisi dhamira ya Mamlaka katika kuunga mkono jitihada zinazolenga kumwezesha mwanamke, kujenga mazingira bora ya kazi na kukuza ustawi wa jamii.