UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KIBAHA HADI KISARAWE
UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KIBAHA HADI KISARAWE
10.2.2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wanaohudumiwa na Mtambo wa Uzalishali Maji Ruvu Juu kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya Majisafi kwa wastani wa Saa 9.
Siku: Jumatano 11 Februari, 2026.
Muda: Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 12:00 Jioni
Sababu: Kuruhusu matengenezo Kinga yatakayofanywa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) katika Kituo cha kupooza umeme Mlandizi
Maeneo yatakayoathirika ni;
Ruvu, Vigwaza, Mlandizi, Visiga, Misugusugu, Kongowe, Soga, Tanita, Kwa Mathias, Picha ya Ndege, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Kimara, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kingazi, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe
Mamlaka inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Wasiliana nasi kupitia
Kituo cha Huduma kwa Wateja 181 (Bila malipo) na 0735 202121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
