Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
USIFUNGE PAMPU KWENYE MITA YA MAJI
04 Sep, 2025 Pakua
USIFUNGE PAMPU KWENYE MITA YA MAJI

USIFUNGE PAMPU KWENYE MITA YA MAJI

Usifunge Pampu ya kuvuta Maji mbele au nyuma ya Mita yako. Kwakufanya hivyo utasababisha yafuatayo:

1. Kuvuruga msukumo wa upatikanaji wa maji kwa majirani zako.

2. Kusababisha majirani zako kukosa huduma ya Maji.

3. Kuharibu Mita/kupunguza ufanisi wa Mita.

ADHABU;

Sheria ya huduma za Majisafi na Usafi wa Mazingira No.5/2019 kifungu namba 61 kinazuia uharibifu wa miundombinu ya Maji. Ukipatikana na hatia adhabu yake ni faini kuanzia Tsh 500,000 hadi Tsh 50,000,000 na/au kifungo kuanzia Miaka miwili hadi Mitano.