Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
CPA RITHAMARY LWABULINDA KUFUATILIA HUDUMA YA MAJI MAPINGA
31 Oct, 2024
CPA RITHAMARY LWABULINDA KUFUATILIA HUDUMA YA MAJI MAPINGA

Mkurugenzi wa huduma kwa wateja ,Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) CPA(T) Rithamary Lwabulinda amekagua hali ya upatikanani wa huduma katika Mkoa wa kihuduma DAWASA Mapinga na kuongea na Wateja wa Mamlaka ili kubaini changamoto zao za kihuduma.

Ametembelea eneo la Kilemela ambapo kulikuwa na changamoto ya huduma  iliyosababisha Wananchi  kukosa huduma ya maji na kushuhudia maboresho ya Miundombinu ikiendelea ya ufungaji wa  pampu itakayosaidia kuongeza msukumo wa maji kwa wateja takribani  73 waliokuwa wanapata maji  kwa kiwango kidogo.

DAWASA Mapinga inahuduma wananchi wa Kata za Mapinga, Kerege na Pangani zenye jumla ya Vitongoji 19 na wakazi  87,418