Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA ILIVYOSHIRIKI MEI MOSI
07 May, 2025
DAWASA ILIVYOSHIRIKI MEI MOSI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeungana na Taasis za Serikali na Binafsi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’ yaliyofanyika katika ngazi ya Mkoa viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Albert Chalamila, yalibeba kauli mbiu "Uchaguzi mkuu 2025 utuletee viongozi wanaojali na kuthamini haki na maslahi ya wafanyakazi, sote tushiriki."

Katika maadhimisho hayo, DAWASA imejitokeza kwa kishindo kwa kuonesha mafanikio katika usimamizi na uboreshaji huduma za Majisafi na Usafi wa mazingira kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani. 

Maadhimisho hayo yamehudhuliwa na maelfu ya Wafanyakazi kutoka Sekta na Taasisi mbalimbali yaliyotanguliwa na maandamano, burudani na hotuba kutoka viongozi wa vyama vya wafanyakazi.

Katika hotuba yake, Mheshimiwa Chalamila amewataka wafanyakazi wote kufanya kazi kwa weledi huku wakitambua dhamana waliyonayo kwa jamii na Serikali ni kufanya kazi kwa bidii