DAWASA YABAINISHA MAMBO MATATU SULUHU YA MAJI GOLANI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imekutana na kuzungumza na wananchi wa Mtaa wa Golani, Kata ya Kimara, Wilaya ya Ubungo kwa lengo la kutatua changamoto ya upatikanaji huduma ya maji mtaani hapo.
Akizungumza kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Everlasting Lyaro amewatoa hofu wananchi wa Golani akiwaambia Mamlaka inatambua changamoto ya maji katika mtaa huo na zipo hatua za muda mfupi na mrefu ambazo zitachukuliwa kuhakikisha kila mwananchi anapatiwa huduma ya majisafi.
"Kwanza tuwaombe radhi wananchi wa hapa Golani kwa changamoto ya maji mnayoipitia, tunatambua maji ni haki ya kila mmoja wetu kupata, Mamlaka inatambua changamoto hii na hapa leo tumekuja kuwaeleza hatua tatu tutakazochukua kutatua changamoto ya maji hapa Golani," amesena Ndugu Lyaro
Lyaro amesema kwa kuanza Mamlaka italeta matenki 5 yenye ujazo wa Lita 10,000 kila moja na kuyajaza maji yatakayouzwa kwa bei elekezi zoezi litakalofanyika mapema tarehe 15.1.2025 oli kukabiliana na changamoto hiyo, lakini pia tutaratibu mgao wa maji katika eneo hili ambapo watapata maji mara tatu kwa wiki, Alhamisi, Jumapili na Jumatatu.
Katika hatua ya mwisho Lyaro ameongeza utatuzi wa changamoto hiyo ya maji utatatuliwa kwa mpango wa muda mrefu wa kujenga kituo cha kusukuma maji eneo la kwa mama Stela na kusaidia maji kufika sehemu mbalimbali zilizookua hazipati huduma awali.
Kwa upande wake, Meneja wa Mkoa wa kihuduma DAWASA Kinyerezi amesema watumishi hawatakaa ofisi bala watatoka kuwafikia wananchi na kuhakikisha yaliyopangwa katika kikao hicho yanatekelezwa.
Ndugu Rajabu Said, Mkazi wa Golani ameshukuru jitihada zinazofanyika kuhakikisha changamoto ya maji mtaani hapo inakwisha na sasa wanaanza kupata matumaini tena ya huduma ya maji na kuondokana na ununuzi wa maji kwa watoa huduma binafsi unaowagharimu fedha nyingi.
