Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA YAENDELEA NA UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA MAJI KOROGWE
04 Feb, 2026
DAWASA YAENDELEA NA UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA MAJI KOROGWE

Fundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) akiendelea na kazi ya matengenezo ya miundombinu katika bomba la inchi 8 eneo la Kimara Korogwe kwa lengo la kudhibiti upotevu wa maji.

Kukamilika kwa matengenezo hayo, kutaimarisha msukumo wa maji  kwa wakazi wa maeneo ya Korogwe Resort, Bucha, Kimara Baruti, Conner na Kibo.

Aidha, Mamlaka inaendelea kuwasihi wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbali za upotevu wa maji, wizi wa mita na maji katika maeneo yao ili kuimarisha utoaji wa huduma, kwa kupiga simu kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 181 (Bure).