Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA YAIMARISHA UPATIKANAJI WA MAJI SHULENI CHALINZE
13 Nov, 2026
DAWASA YAIMARISHA UPATIKANAJI WA MAJI SHULENI CHALINZE

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetimiza ahadi ya kupeleka tanki la maji iliyotoa siku ya Mahafali ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Chalinze iliyopo Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, ikiwa ni juhudi za kuunga mkono shughuli za utunzaji wa mazingira kupitia klabu ya mazingira ya shule hiyo.

Utekelezaji wa ahadi hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa ushirikiano kati ya DAWASA na jamii, hususani Taasisi za elimu, katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira na matumizi sahihi ya rasilimali za maji. Kupitia msaada huo, DAWASA inalenga kuimarisha mazingira ya kujifunzia na kuwezesha wanafunzi kuwa na uelewa zaidi kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa maji.

Aidha, tanki hilo litasaidia shule kuwa na uwezo wa kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kila siku, hivyo kuongeza urahisi wa upatikanaji wa maji ambao utaboresha usafi wa mazingira na afya za jamii iliyopo shuleni hapo.