DAWASA YASHIRIKI UZINDUZI MRADI WA MAJI BUTIMBA - MWANZA

Katika kuunga mkono juhudi za serikali, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeshiriki kwenye ziara ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Butimba uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Mkoani Mwanza wenye thamani ya shilingi billioni 70.
Katika kuunga mkono jitihada hizo nzuri na kubwa zilizofanywa na Wizara ya maji, DAWASA imejumuika na Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya maji kwenye matukio haya makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita.
Ushiriki wa DAWASA ni muendelezo na utamaduni mzuri wa kupongezwa kwani unaonyesha na kuhuisha maana halisi ya "team work" kwenye utumishi wa umma.
Ziara hiyo kwa upande wa Wizara ya maji iliongozwa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso na Katibu Mkuu wa Wizara ya maji Mhandisi Mwajuma Waziri pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka na Taasisi za maji nchini na watumishi wengine wa Wizara na taasisi zilizopo chini ya wizara ya maji.