DAWASA YATAMBUA MCHANGO WA MWALIMU NDIMANGWA NZOTA KATIKA MALEZI NA ELIMU KWA JAMII
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inapenda kukushukuru kwa dhati kwa ushirikiano wako wa karibu na Mamlaka katika shughuli mbalimbali za kulea, kuhudumia na kuelimisha Jamii ya Wanafunzi Shule ya Sekondari Pugu.
Kupitia ushirikiano wetu, tumejifunza umuhimu wa kuunganisha nguvu katika kuleta mabadiliko chanya na kugusa maisha ya wengi.
Asante kwa kuwa sehemu ya safari ya Mamlaka ya kujali na kusaidia Jamii yenye changamoto. Ingawa safari yako ya utumishi imefikia tamati, mchango wako na kumbukumbu nzuri ulizoacha vitaendelea kuishi katika mioyo ya wengi.
Hongera kwa kustaafu, Mwalimu Ndimangwa Nzota, DAWASA inakutakia kila la heri katika maisha yako mapya ya baada ya utumishi na asante kwa mchango wako katika kulea Wanafunzi.
