DAWASA YATETA NA WAFANYABIASHARA KARIAKOO WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA
07 Oct, 2026
Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) wameadhimisha wiki ya huduma kwa Mteja kwa kutembelea Wafanyabiashara katika soko la Kariakoo Jijini Dar es salaam na kutoe elimu ya usafi wa Mazingira na umuhimu wa kulinda miundombinu ya Majitaka kwa kutotupa taka ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko yanayoweza kusababishwa na kuziba kwa miundombinu ya majitaka.
Wiki ya huduma kwa Mteja inaadhimishwa kila tarehe 5 hadi 9,Oktoba na kauli mbiu ya Mwaka huu inasema "Kwenda Hatua zaidi".
