DAWASA YAWAFIKIA WATEJA KUHAMASISHA MAKUSANYO MAGOMENI

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa kihuduma Magomeni wanaendelea na zoezi la kuhamasisha wananchi kufanya malipo ya huduma za maji hususani kwa wateja wenye madeni ya maji ya muda mrefu ili waendelee kupata huduma pasipo kusitishiwa.
Zoezi limetekelezwa katika mitaa mbalimbali ikiwemo Magomeni Kagera, Mwembe chai, Magomeni usalama, Makurumla, Kimamba na Manzese huku likienda sambamba na utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya maji, utunzaji wa vyanzo vya maji, ulinzi wa miundombinu ya maji, umuhimu wa kulipa bili za maji kwa wakati pamoja na kusitisha huduma kwa wateja wenye malimbikizo ya madeni.
Mamlaka inasisitiza wananchi na wateja wa DAWASA katika maeneo yote ya kihuduma kulipa bili zao kwa wakati ili kuepukana na usumbufu wa kusitishiwa huduma kutokana na bili kutolipwa kwa wakati.