PAMPU MPYA YALETA TUMAINI HUDUMA YA MAJI KISUKURU
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imetekeleza zoezi la ufungaji wa pampu mpya katika kituo cha kusukuma maji (Booster pump) kilichopo Segerea kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa Maji kwa baadhi ya mitaa ya kata ya Kisukuru inayopokea Maji kutoka Kituo hiko.
Mhandisi Phylemon Ojode kutoka mkoa wa kihuduma DAWASA - Tabata amesema zoezi la ufungaji wa pampu hiyo limetekelezwa baada ya pampu iliyokuwepo awali kupata hitilafu na kupelekea huduma kutokuwa ya uhakika ambapo pampu mpya iliyofungwa ina uwezo wa kusukuma zaidi ya lita 160,000 kwa saa na msukumo mzuri, hali inayoleta matumaini ya kuyafikia pia maeneo yenye miinuko.
"Uboreshaji huu unatarajia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ndani ya kata ya Kisukuru na baadhi ya mitaa ya kata ya Segerea kwa kuongeza hali ya upatikanaji wa maji kwa kiasi kikubwa na kuongeza msukumo wa maji katika maeneo hayo". Ameeleza mhandisi Ojode.
Zoezi hili la maboresho ya kubadilisha pampu limefanyika ili kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa maji katika maeneo ya Kokomtama, Viwanja vya bank, Magoza shule, Magoza Serikali ya Mtaa, Nobo college, ACCT, Mtaa wa Nyela, Arafa, msikiti wa Mangara, Arafa Mianzini, Kwa Mpuruti, Sabisa, Kwa Sanga, Mashilingi butcher, Gasper Mrema, Mtaa wa Mtoni, Efatha
