Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
HONDOGO MAJI NI UHAKIKA, WATENDAJI DAWASA WAPONGEZWA
12 Feb, 2026
HONDOGO MAJI NI UHAKIKA, WATENDAJI DAWASA WAPONGEZWA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea kusisitiza usomaji wa dira za maji shirikishi ili kupunguza dhana ya baadhi ya wateja kuhusu kubambikiziwa bili za maji kila mwezi zisizo akisi matumizi yao.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa DAWASA mkoa wa kihuduma Kibamba Ndugu Barnabas Taligunga wakati alipotembelea wateja wa kata ya Kibamba na kushiriki nao kwa pamoja zoezi usomaji wa dira hizo za maji na kupokea mrejesho wa hali ya huduma ya maji katika maeneo hayo.

"Kama mnavyoelewa utaratibu wa DAWASA zoezi la usomaji wa dira za maji huanza kila tarehe 10 hadi 15 kila mwezi na zoezi hili ni shiriki hivyo leo tumetembelea wateja katika mitaa ya Hondogo, Kibwegere na Kibamba, tumesoma pamoja na tumetoa elimu zaidi ya usomaji wa dira za maji" alisema Taligunga

Naye Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Hondogo, Ndugu Leonard Sabuni amepongeza jitahada za Mamlaka katika kushirikisha wananchi kata zoezi la usomaji wa dira maji ambapo hupunguza malalamiko ya ubambikiziwaji bili za maji kwa baadhi ya wateja, nakutoa rai kwa wananchi kulipia bili zao za maji kwa wakati ili kuwezesha kuimarisha utoaji wa huduma bora.

"Kwa kweli sasa DAWASA imebadilika tunashukuru mtoka mnakuja mitaani kuangalia huduma ilivyo na mnatushirikisha viongozi wa serikali hata ikifika wakati huu wa usomaji wa dira za maji, jitihada zaidi ziongezwe katika kuhamasisha matumizi sahihi ya huduma ili kila mwananchi afaidike na huduma ya maji" alisema Sabuni

Mkoa wa kihuduma DAWASA Kibamba unahudumia jumla ya wateja 32,150 katika kata tano ambazo ni Kwembe, Kibamba, Kiluvya, Msigani na Mbezi.