KIBAHA, VISIGA, MTAMBANI NA KILANGALANGA WAITWA KUUNGANISHIWA HUDUMA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea kusogeza huduma ya maji wananchi kwa kuwaunganishia wakazi takribani 100 wa maeneo ya Mwendapole, Mtambani, Kilangalanga na Kichangani ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuboresha huduma za kijamii.
Zoezi hilo limetekelezwa kupitia ofisi za DAWASA Kibaha, ambapo wateja kutoka Kata za Kibaha, Kilangalanga, Mtambani na Visiga wamekabidhiwa vifaa na kufungiwa huduma za Maji.
Kupitia zoezi hilo pia DAWASA imetoa elimu kwa Wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza miundombinu ya maji, kulipa bili kwa wakati na kushiriki katika kudhibiti upotevu wa maji ili kuhakikisha huduma inaendelea kuwa endelevu.
Wananchi wamehimizwa kuendelea kushirikiana na mamlaka hiyo kwa kutoa taarifa kuhusu changamoto za huduma na kupata ufafanuzi kupitia namba 0735 451 875 (DAWASA KIBAHA) au 181, namba ya huduma kwa wateja inayopatikana bila malipo.
