Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
KIBONDEMAJI WABORESHEWA HUDUMA YA MAJI
10 Jun, 2025
KIBONDEMAJI WABORESHEWA HUDUMA YA MAJI

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) mkoa wa kihuduma Mbagala wakiendelea na kazi ya uboreshaji huduma ya maji kwa wakazi wa kata ya Kibondemaji katika Wilaya ya Temeke.

Akizungumzia maboresho hayo Meneja DAWASA Mbagala, Julieth John amesema lengo la kazi hiyo ni kuboresha hali ya upatikanaji wa maji katika baadhi ya maeneo ya kata ya Kibondemaji ambayo wananchi wamekuwa wakikosa huduma kwa muda.

"Kuna baadhi ya maeneo ya kata hii ya Kibondemaji yamekuwa hayana huduma ya maji ya uhakika ila tumeweza kulaza bomba ili tuweze kuongeza msukumo wa maji kwa maeneo yaliyokuwa hayapati maji." amesema ndugu Julieth

Aidha kazi hiyo imehusisha ulazaji wa bomba za inchi 2 kwa umbali wa mita 300 ambazo zinatarajia kunufaisha wakazi takribani 500 wa maeneo ya Mchikichini, Kibondemaji kwa Walimu na Kibondemaji B.