KICHANGANI WABORESHEWA HUDUMA YA MAJI
17 Jul, 2025

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa kazi wa Kihuduma Kigamboni inafanya maboresho ya miundombinu ya bomba la inchi 2" kwa umbali wa mita 480 katika eneo la Kichangani katika Kata ya Kisarawe II Wilaya ya Kigamboni.
Maboresho hayo yanahusisha ulazaji wa mabomba ya inchi 2" kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji kwa Wananchi waliokuwa wanapata changamoto ya upatikanaji wa huduma kwa ufanisi.
Kukamilisha kazi hiyo kutaongeza msukumo wa maji kwa Wananchi takribani 350 katika maeneo ya Kichangani,Yadi, Kiwanda Cha maandazi na Zahanati