KIMBWENDE WABORESHEWA HUDUMA ZA MAJI
21 Sep, 2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa kazi wa DAWASA Kibaha imeendelea na kazi ya kuboresha miundombinu ya majisafi katika Mtaa wa Kibwende, Kata ya Mihande, Mji wa Mlandizi mkoani Pwani itakayowanufaisha wakazi takribani 700.
Maboresho hayo yanayohusisha bomba la inchi 8 yanalenga kuimarisha usambazaji wa maji pamoja na kupunguza upotevu wa maji ili kuongeza upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
DAWASA inaendelea kuwasihi wananchi kutoa taarifa za uvujaji na upotevu wa maji katika maeneo yao ili kulinda rasilimali ya maji na kuboresha huduma
