Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
KINYEREZI YATOA RAI ULIPAJI BILI KWA WAKATI
22 May, 2024
KINYEREZI YATOA RAI ULIPAJI BILI KWA WAKATI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma DAWASA - Kinyerezi imewakumbusha wateja kulipa ankara zao za mwezi kwa wakati ili kuwezesha Mamlaka kuboresha zaidi huduma zake.

Mkoa wa Kihuduma DAWASA-Kinyerezi unahudumia wateja takribani 6,646 katika kata 9 za Kinyerezi, Ukonga, Gongolamboto, Kipawa, Kwembe, Bonyokwa, Pugu Station, Saranga na Msigani.

Meneja wa DAWASA Kinyerezi, Ndugu Burton Mwalupaso amesema kuwa kwa mujibu wa mkataba wa huduma kwa wateja, Mteja ana wajibu wa kulipia ankara yake ya Maji kulingana na matumizi yake ya mwezi husika

"Sisi kama DAWASA tuna wajibu wa kuhakikisha huduma inafika kwa mteja na kuhakikisha taarifa sahihi zinatolewa kwa mteja, hivyo ni vyema wateja  kukumbuka umuhimu wa kulipia huduma kwa wakati sahihi ili kuwezesha shughuli hii kuwa endelevu," amesema. 

Ndugu Mwalupaso ameeleza kuwa DAWASA inatekeleza miradi mingi ya kimkakati ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ambayo inakusudia kufikisha lengo la kuwafikia wananchi waishio mijini kwa asilimia 95 ifikapo 2025.

"Tumefanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati hivyo nitoe rai kwa wateja wetu kulipia huduma kwa wakati kulingana na matumizi," ameeleza.